MCHUNGAJI, VICTOR GASPER MALAMLA. 1Wakorintho 10:10, "Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu." Yohana 10:10, "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele." Nini maana ya uharibifu?Uharibifu ni roho inayoondoa ukamilifu wa Mungu. Mungu ametuumba wakamilifu, amefanya kila kitu kwa ukamilifu. Anayeharibu na kutoa ukamilifu ni adui (shetani) ili tushindwe kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu. Maana ya pili ya uharibifu ni; roho inayovuruga utaratibu na mpangilio wa Mungu kwenye maisha ya kila siku ya wanadamu. Kazi ya roho ya uharibifu ni kuvuruga mpangilio uliopo, kila mtu anakuwa anafanya anachokitaka yeye. Hata kama ni kanisani kunakuwa na uvunjifu wa mipangilio na miongozo yote iliyopo mahali hapo. Maana ya tatu ya uharibifu ni; roho yenye nguvu ya mauti na kuua, inaua mwili, kazi, elimu, biashara, ndoa na afya. Popote palipo na roho ya uharibifu...
Comments
Post a Comment