Ibada tarehe : 21/8/2021 Somo : UHARIBIFU
MCHUNGAJI,
VICTOR GASPER MALAMLA.
1Wakorintho 10:10, "Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu."
Yohana 10:10, "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele."
Nini
maana ya uharibifu?Uharibifu ni roho inayoondoa ukamilifu wa Mungu.
Mungu ametuumba wakamilifu, amefanya kila kitu kwa ukamilifu.
Anayeharibu na kutoa ukamilifu ni adui (shetani) ili tushindwe kufanya
yaliyo mapenzi ya Mungu.
Maana
ya pili ya uharibifu ni; roho inayovuruga utaratibu na mpangilio wa
Mungu kwenye maisha ya kila siku ya wanadamu. Kazi ya roho ya uharibifu
ni kuvuruga mpangilio uliopo, kila mtu anakuwa anafanya anachokitaka
yeye. Hata kama ni kanisani kunakuwa na uvunjifu wa mipangilio na
miongozo yote iliyopo mahali hapo.
Maana
ya tatu ya uharibifu ni; roho yenye nguvu ya mauti na kuua, inaua
mwili, kazi, elimu, biashara, ndoa na afya. Popote palipo na roho ya
uharibifu kunakuwa na mauti. Ukiona kila unachofanya hakisongi mbele
basi ujue kuna uchawi ndani yake
Anaeharibu
anaitwa mharabu. Shetani anatenda kazi katika roho ya uharibifu, ili
uharibifu wa shetani utokee kwenye kazi, biashara, taifa, elimu na
mahali popote kitendea kazi chake ni uchawi. Uharibifu na uchawi ni
vitu vinavyoenda sambamba. Mtu anayefanya kazi na shetani anaweza
kufanya uharibifu mahali popote. Mtu mchawi anaweza akaenda kanisani na
kunena kwa lugha kama wengine, lakini kwa mganga ni ngumu sana. Kuna
mahali hawezi kwenda na akienda mahali hapo basi kazi zake zote
zinaharibika.
Muhimu kufahamu ni;
-Uganga ni kiwango cha chini cha uchawi, waganga wote wanaripoti kwa wachawi.
-Matambiko ni uchawi.
- Mila na desturi ni uchawi. Uchawi umebeba vipengele vingi sana ndani yake.
Ukiona
mtu anatamani kuacha uzinzi, kiburi, hasira, uasherati, ulevi na
masimango na hawezi basi ujue kuna uchawi ndani yake. Kiburi ni chanzo
cha mafarakano na migogoro katika ndoa nyingi. Uchungu
ni roho ambayo inatumwa kwa mtu ili ashindwe kusamehe, na mtu
akishindwa kusamehe basi hawezi kusamehewa na hapo anakuwa amefungua
mlango kwa ajili ya adui kupandikiza mateso kwake.
Kushinda
vita vya kichawi ni lazima ushughulike na moyo kwanza. Na jambo hili
sio la siku moja anayeweza kukusaidia ni Roho Mtakatifu, mwambie
akufundishe kusamehe na uondokane na hali ya kutokusamehe (gubu). Sio
kila tabia ambayo mtu anayo ni ya kwake zingine zinatokana na uchawi.
ILI UWEZE KUSHINDA UCHAWI NI LAZIMA;
1.
Uepukane na uchungu, jifunze kuwa mtu wa kusamehe na kuachilia watu kwa
kadri unavyowashikilia watu ndivyo unavyozidi kufungua mlango kwa ajili
ya mateso, magonjwa na maumivu mengi kwako. Ni lazima uweze kuutiisha
mwili wako ili uweze kukutana na Roho wa Mungu.
2Wakorintho 5:17, "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya."
Kiumbe kipya ni roho yako, kazi ya uchawi ni kupambana na roho yako ili isiweze kushabihiana (kuendana) na mwili wako.
Ili
yale unayoyaona katika roho yadhihirishwe katika damu na nyama ni
lazima ushinde uchawi. Bila mtu kuushinda uchawi hawezi kufikia makusudi
ya Mungu.
2. Kufunga na
kuomba ni lazima ili uweze kuushinda uchawi. Hauwezi kukwepa kufunga na
kuomba kama unatamani kufikia makusudi ambayo Mungu ameweka kwako.
Mtu
asipofanya maamuzi ya kuutisha mwili wake kuushinda uchawi ni ngumu
mno. Hauwezi kwenda mbinguni ukaketi kama haujashinda hapa duniani. Kila
mwamini lazima aoneshe ushindi wake kupitia Yesu.
Mika 5:12-15, "nami nitakatilia mbali uchawi, usiwe mkononi mwako; wala hutakuwa tena na watu wenye kutabana..."
Kuna mambo manne MUNGU anashughulika nayo;
1. Anashughulika na roho zote za uchawi.
2. Anashughulika na sanamu na nguzo, vitu ambavyo vinatunza uchawi.
3. Anavunja madhabahu na kukomesha kazi zao.
4. Anashughulika na watu wanaotenda au kumiliki huo uchawi.

Comments
Post a Comment