IBADA YA JUMAPILI TAREHE 28.08.2022, SOMO : ROHO YA UCHAWI
MCHUNGAJI VICTOR GASPER MALAMLA
Wagalatia 3:1-3, "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?.."
Ili mwamini aweze kushinda roho ya uchawi ndani yake ni lazima
1. Ajifunze kutii kwa ukamilifu ndani yake. Wachawi wanapata nafasi kwa watakatifu kutokana na kushindwa kuwa watii. Kutokana na kiwango cha utii ulichonacho unaweza kufukuza mapepo kila mahali. Muda mwingine hauitaji kuomba ila kwa utii wako tu unaweza kushinda. Kwa kadri unavyoelekezwa na kutii, unaweza kutiisha kila kitu yani viumbe hai na visivyo hai. Usipokuwa mtii kwenye mapato, hauwezi kupata mafanikio. Ili Mungu akupe baraka zinazokutofautisha na wengine ni lazima uwe mtii katika mapato. Hapo ulipofikia leo ni kwa sababu neema ya Mungu ni kubwa na imekufikisha hapo.
Isaya 1:19, "Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;"
Ukiona umeokoka halafu ghafla unakutana na changamoto nyingi, ujue kwamba Mungu anakukumbusha ili umrudie yeye. Watu wengi wamekuwa wakipitia changamoto nyingi kutokana na kujisahau. Mfano mtu alikuwa anatoa fungu la kumi kwa uaminifu lakini baada ya mapato yake kuongezeka anaanza kumwibia Mungu. Ila kwa kuwa Mungu wetu ni wa haki huwa anakukumbusha na kukupa moyo wa toba ili urudi mwanzo.
Mithali 3:12, "Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi, kama vile baba mwanawe ampendezaye."
2. Amjue Mungu wa kweli, na hili litathibitishwa na matunda ya matendo yake. Kwa kumjua Mungu utafanya yaliyo mapenzi yake na kutembea katika kweli yake. Tunamjua sana Mungu kupitia neno lake, kupitia neno lake tunaweza kushinda kushinda nguvu zote za adui kutokana na ufahamu ambao tunaupata.
Danieli 11:32, "Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu."
Makanisa mengi kwa sasa wamekuwa wakizungumzia sana kwa habari ya fedha na mali. Wamesahau kuhubiri kwa habari ya kweli ya Mungu. Hii inafanya uharibifu uzidi kuwa mkubwa ndani ya kanisa. Kwa sasa ndoa za jinsia moja na ushoga vimezidi kwa kiwango cha juu. Malezi kwa watoto yamekuwa mabaya, wazazi wamekuwa chanzo cha watoto kuharibika. Vifungo vingi na maumivu mengi ni matunda ya matokeo ya wazazi wetu. Tulikuta wazazi wanataabika na sisi tunapita katika yale ambayo wamepitia. Ila wewe ukishaoka na kutambua hili hakikisha unatoka katika vifungo hivyo ili uzao wako uwe salama.
Uchawi unaweza kusababisha hata ukikutana na mtu wa hatma yako anakuona ni mtu ambaye upo kwa ajili ya kumpotezea muda. Pia roho hii imeingia na kuvuruga ndoa na familia nyingi. Wanawake wanafanya mambo ambayo yanapelekea kudharau waume zao na wao kuonekana kama vichwa vya familia. Kutokana na kushindwa kutii maovu mengi yanaongezeka na familia nyingi zinapitia mateso na maumivu mengi.
KANISA LA EFATHA NUNDU MWANZA


Comments
Post a Comment