Posts

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 28.08.2022, SOMO : ROHO YA UCHAWI

Image
                  MCHUNGAJI VICTOR GASPER MALAMLA Wagalatia 3:1-3, "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?.." Ili mwamini aweze kushinda roho ya uchawi ndani yake ni lazima   1. Ajifunze kutii kwa ukamilifu  ndani yake. Wachawi wanapata nafasi kwa watakatifu kutokana na kushindwa kuwa watii. Kutokana na kiwango cha utii ulichonacho unaweza kufukuza mapepo kila mahali. Muda mwingine hauitaji kuomba ila kwa utii wako tu unaweza kushinda. Kwa kadri unavyoelekezwa na kutii, unaweza kutiisha kila kitu yani viumbe hai na visivyo hai. Usipokuwa mtii kwenye mapato, hauwezi kupata mafanikio. Ili Mungu akupe baraka zinazokutofautisha na wengine ni lazima uwe mtii katika mapato. Hapo ulipofikia leo ni kwa sababu neema ya Mungu ni kubwa na imekufikisha hapo. Isaya 1:19, "Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;" Ukiona umeokoka halafu ghafla una...

Ibada tarehe : 21/8/2021 Somo : UHARIBIFU

Image
  MCHUNGAJI,   VICTOR GASPER MALAMLA.   1Wakorintho 10:10, "Wala msinung’unike, kama wengine wao walivyonung’unika, wakaharibiwa na mharabu." Yohana 10:10, "Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele."   Nini maana ya uharibifu?Uharibifu ni roho inayoondoa ukamilifu wa Mungu. Mungu ametuumba wakamilifu, amefanya kila kitu kwa ukamilifu. Anayeharibu na kutoa ukamilifu ni adui (shetani) ili tushindwe kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu.   Maana ya pili ya uharibifu ni; roho inayovuruga utaratibu na mpangilio wa Mungu kwenye maisha ya kila siku ya wanadamu. Kazi ya roho ya uharibifu ni kuvuruga mpangilio uliopo, kila mtu anakuwa anafanya anachokitaka yeye. Hata kama ni kanisani kunakuwa na uvunjifu wa mipangilio na miongozo yote iliyopo mahali hapo.  Maana ya tatu ya uharibifu ni; roho yenye nguvu ya mauti na kuua, inaua mwili, kazi, elimu, biashara, ndoa na afya. Popote palipo na roho ya uharibifu...

Ibada Tarehe 14/8/2022, SOMO : UONGOZI

Image
 Mchungaji , VICTOR GASPER MALAMLA + Yohana 14:16-18, "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;.." Kabla ya kuanza jambo lolote hakikisha unakaribisha uwepo wa Roho Mtakatifu. Kuna sauti ya Mungu baba, Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu, Wote wanaongea ila anaeweza kutafsiri ni Roho Mtakatifu. Ukishaokoka anaekaa ndani yako ni Roho Mtakatifu na yeye ndiye anayetukumbusha kwa habari ya toba na rehema pale tunapokosea. Roho Mtakatifu ndiye msaidizi na kiongozi wetu, bila yeye hatuwezi kufika popote.   + 1 Timotheo 3:1 -Ni neno la kuaminiwa;  mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema..." Uongozi unaanzia nyumbani, Mtoto inabidi umlee katika malezi ambayo hata akikua atakukumbuka kwa kumfanya kiongozi bora. Hata kama umesoma sana kama haujasoma uongozi ni ngumu sana kufikia malengo yako na ubaadae wako. Kila aliyeumbwa na Mungu anachembechembe za uongozi ndani yake. Kazi yetu ni kuichochea ile mbegu ili itoe matunda mazuri. Hauw...